Jukumu la Ujerumani katika Matukio ya Siku za Mwisho
Uvamizi wa Urusi katika nchi ya Ukraine mwaka 2022 umeshangaza Ulimwengu.
Tishio la Putini kutumia mabomu ya Nyuklia limeamsha hofu ya vita ya tatu ya Dunia. Hivi karibuni Kansela wa Ujerumani ameahidi kutumia Euro Billioni 100 kwa ajili ya kuliimarisha Jeshi la Ujerumani. Mataifa mengi ya Ulaya yameanza kutafuta kujiunga na Umoja wa Nchi za Ulaya na NATO.
Haya matukio yanaelekea wapi?
Je, Unabii wa Biblia unasemaje kuhusu wakati ujao wa Ulaya, Urusi na Dunia?
Siku za Mwisho na Babeli
Kitabu cha Ufunuo kinazungumzia mji mmoja mkubwa uitwao “Babeli” wenye “ufalme juu ya wafalme wa nchi” katika nyakati za mwisho (Ufunuo 17:5,18). Hii “Babeli” inawakilisha nguvu ya kisiasa, kiuchumi na dini ambayo itakuja kuutawala ulimwengu mara kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo (Ufunuo 18).
“Babeli” ya wakati wa leo ipo sehemu gani?
Je, utawala huu wenye nguvu ya kisiasa na dini utatokea lini kwenye uso wa dunia?
Jibu lipo katika kitabu cha Daniel 4.
Unabii huu unafunua ya kuwa Babeli tayari ipo.
Mwisho wa somo hili, tafadhali tumia muda wako usome Daniel 4. Kwasasa, huu hapa muhtasari wake: Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliota ndoto kuhusu mti mrefu unaotoa kivuli na chakula kwa ndege wote na Wanyama wote duniani. Halafu ule mti ukakatwa, na shina lake likaachwa aridhini pamoja na pingu ya chuma na shaba hata nyakati saba zipite juu yake.
“Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake; tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala”. (Daniel 4:23-26)
Baada ya mwaka mmoja unabii huu ulitimia. Mungu akamfanya Nebukadreza awe kichaa kama adhabu ya kiburi chake. Hata baada ya miaka saba, fahamu za Mfalme zikamrudia na akarudi kutawala ufalme wa Babeli.
Kwanini unabii huu upo kwenye Biblia?
Fahamu ya kuwa, Daniel hakuandika unabii huu mpaka pale ulipotimia. Kwahiyo, unabii huu hautuambi chochote cha wakati ujao—isipokuwa ulitabiri utimilifu wa pili kutokea badae. Na kweli, utimilifu wa pili ulitokea.
Kama ilivyokuwa Babeli ikakosa mtawala kwa “nyakati” saba, wakati Nebukadreza amepoteza fahamu zake, ulikuja wakati wa pili ambapo Babeli alikosa mtawala kwa “nyakati” saba. Na nini maana ya “wakati”?
Katika unabii wa kibiblia, “nyakati” inamaanisha ni kipindi cha siku 360. Tunajuaje? Ufunuo 11:2-3 inataja kipindi cha nyakati cha “miezi 42” na siku “1260”. Katika ufunuo 12:14 kipindi cha nyakati kama hizo kinatajwa kuwa “wakati na nyakati na nusu ya wakati” (1 + 2 + 1/2 = 3 1/2 nyakati). Kama ukifanya mahesabu vizuri utaona kuwa “wakati” ni siku 360.
Kuelewa utimilifu wa pili wa Daniel sura ya 4, inabidi pia ujue katika unabii wa Biblia, “siku” huwa inawakilisha mwaka mmoja. Soma Hesabu 14:34 na Ezekieli 4:6 kuhakikisha hili.
Katika utimilifu wa kwanza wa unabii katika kitabu cha Daniel sura ya 4, Babeli ilikosa kuwa na kiongozi kwa siku 2520 (7 x 360 = 2520), ambayo ni miaka saba.
Katika utimilifu wa pili, Babeli ilikosa kiongozi kwa siku 2520. Mungu aliukata utawala wa Babeli na kuweka pingu ya chuma na shaba kwenye shina lake ili kuuzuia usimee kwa muda wa siku 2520. Lakini majira yalipotimia ya hizo “nyakati saba”, Mungu aliondoa pingu ya chuma na shaba. Na kwa wakati ule, mtawala mpya akaingia madarakani na “Babeli” ambayo inaelezwa kwenye kitabu cha ufunuo ikaanza kukua tena. Hii “Babeli” inazidi kukua tena mbele ya macho yetu-na itaendelea kukua mpaka itatawala dunia yote.
Hii ilitokea lini?
Fahamu ya kuwa, mara tu baada ya ndoto ya Nebukadreza katika Daniel sura ya 4, sura inayofuata imeelezea kuhusu anguko la utawala wa Babeli (kama ilivyo baadhi ya nabii za Biblia, kitabu cha Daniel kimepangiliwa kuonyesha ujumbe maalumu Zaidi ya kuonyesha mtiririko wa wakati). Wakati watawala wa Babeli wakiwa wanafanya sikukuu, mkono ulitokea na kuandika ujumbe kwenye ukuta. Mfalme alimuita Daniel asome ujumbe huo na kuufafanua. Danieli akaeleza ya kuwa ujumbe huo kwenye ukuta unamaanisha ya kuwa Ufalme wa Babeli umefika mwisho, na Mungu amewapa Wamedi na Waajemi.
Hakika, Wamedi na Waajemi wakautawala Ufalme, na wakauvamia mji wa Babeli usiku uo huo. Tunaweza tukapata wakati halisi wa tukio hilo lililoandikwa katika kumbukumbu ya Nabonidus, inayosema: “Siku ya kumi na nne Sipa ilichukuliwa bila ya vita. Nabonidus akakimbia. Siku ya kumi na sita, Ubaru, gavana wa Gutiamu, na jeshi la Sairasia, bila ya vita wakaingia na kutawala Babeli.”
Sipa ikachukuliwa siku ya kumi na nne ya wababeli mwezi wa Tishiritumu, mwaka 539 kabla ya Kristo. Baada ya siku mbili, Danieli akawaambia watawala wa Babeli ya kuwa Babeli imeshachukuliwa na Wamedi na Waajemi, na usiku uo huo mji wa Babeli ukaanguka. Kwahiyo kutokea hapo, tunapata muda halisi wa mwanzo wa 2520-kipindi cha miaka ambayo Babeli atakuwa hana Kiongozi.
Kabla hatujafanya mahesabu ya kujua muda halisi ambao kipindi hicho kiliisha, elewa ya kuwa tunapata maelezo mengine ya kipindi hiki cha miaka 2520 katika maneno yaliyoandikwa kwenye ukuta. Maneno yalikuwa “MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI” (Danieli 5:25). Kama una Biblia yenye maelezo ya chini, utaona haya maneno yakielezwa kama kipimo cha fedha. “Mene” ni mina, ambayo ni shekeli 50. “Tekeli” ni shekeli. “Peresi” ina maana ya kukata katikati au “nusu” na nusu ya mina ni shekel 25. Jumlisha 50 + 50 + 1 + 25 = shekeli 126. Kutoka 30:13 inasema, “shekel ni gera 20”. Zidisha shekeli 126 kwa 20, unapata gera 2520. Na namba hiyo ni sawa sawa na ile namba tuliyoipata katika unabii wa “nyakati saba” kwenye kitabu cha Daniel 4.
Sasa ni muhimu kujua ya kuwa tarehe katika unabii wa Biblia huwa inatumia kalenda ya kiebrania. Mwezi Tishrituma katika kalenda ya Babeli ni sawa na mwezi Tishri katika kalenda ya kiebrania, kwahiyo mjii wa Sippa ulianguka tarehe 14, mwezi Tishri mwaka 539 kabla ya Kristo, na baada ya siku mbili, Daniel akasema ya kuwa Ufalme wa Babeli umepewa Wamedi na Waajemi. Kwahiyo tutaanza kuhesabu kuanzia tarehe 14 ya mwezi Tishri, 539 kabla ya Kristo. Jumlisha miaka 2520 tunapata tarehe 14 ya mwezi Tishri, 1982 baada ya Kristo.
(Unaweza ukauliza, sio kwamba ni kuchukua mwaka 539 kabla ya Kristo + 1982 baada ya Kristo = 2521? Ndio. Lakini huwa hakuna “mwaka 0” kati ya mwaka1 kabla ya Kristo na mwaka 1 baada ya Kristo. Kwahiyo mwaka kati ya mwaka 1 kabla ya Kristo na mwaka 1 baada ya Kristo ulikuwa ni mwaka 1 na sio miaka miwili kama ungechukua mwaka 1 kabla ya Kristo + mwaka 1 baada ya Kristo.)
Ukiangalia kalenda ya kiebrania, utaona ya kuwa tarehe 14 ya mwezi Tishri, 1982, inaangukia tarehe 1 mwezi wa Kumi. Sasa nenda katafute ni nini kilitokea katika tarehe 1/10/1982.
Unapata nini? Kitu Fulani kumuhusu kansela wa Ujerumani? Ni kweli kabisa. Kansela wa Ujerumani ya Magharibi aliondolewa madarakani kwa ghafla na nafasi yake ikachukuliwa na Helmut Kohl—sio kwa uchaguzi, ila ni kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae. Na hii ndio ikawa historia pekee ya Ujerumani ya kiongozi kuingia madarakani kwa njia hiyo isiyokuwa ya kawaida.
Ujerumani itaiongoza Dunia?
Je, ujio wa Helmut Kohl kwa ghafla na bila kutegemewa na akaingia madarakani tarehe 1/10/1982 ilikuwa ni utumilifu wa pili wa unabii katika kitabu cha Danieli4. Angalia michanganuo ifuatayo na kisha uamue mwenyewe.
-
Baada ya miaka minane, chini ya uongozi wa Kohl, Ujerumani ya Mashariki na Magharibi ziliungana katika tarehe na mwezi ule ule ambao Kohl aliingia madarakani: mwezi Tishri14 ambayo ilikuwa tarehe 03/10/1990.
-
Kohl alikuwa ni wakili kiongozi wakati wa muunganiko wa Ulaya ya Mashariki na Magharibi. Alikuwa ni mmoja kati ya wawili waliokuwa waanzilishi wa mchakato wa kuanzisha Umoja wa Ulaya. Mchakato huu ukazalisha Umoja wa Ulaya.Ukaanzisha Euro kama Fedha halisi ya kutumika katika Umoja wa Ulaya, na ukafungua milango kwa nchi nyingine za Ulaya mashariki kujiunga na Umoja wa Ulaya
-
Kohl na warithi wake walifanya Ujerumani kuwa Nchi yenye nguvu Ulaya, na wanafanya kuiweka Ulaya kuwa Nchi yenye nguvu kiutawala Duniani.
Ni kwa nafasi gani ya kwamba huu mfululizo wa matukio utatokea katika siku ile ile ambayo ilitabiriwa miaka 2500 iliyopita?
Kumbuka unabii wa Daniel 4 ya kuwa chuma cha shaba kimewekwa kwenye shina la mti ambao ulikatwa. Na baada ya chuma hicho cha shaba kuondolewa mnamo tarehe 1/10/1982, utawala mpya wenye nguvu Duniani “Babeli” ulianza kuchipua kutoka katika mizizi ya Babeli ya zamani.
Nabii kwenye Biblia zilivuviwa na Mungu-na Mungu anaposema kitu Fulani kitatokea, anahakikisha kinatokea kwa wakati muafaka.
Nani atamiliki karne ya 21?
Ujerumani ikiiongoza Ulaya, pamoja na Taasisi kubwa za kidini, watatimiza unabii wa Biblia kuhusu Babeli na siku ya mwisho.
Unabii wa Biblia unaonyesha kuwa, hii “Babeli” itakuja kutawala Ulimwengu wote, ikiwemo Urusi, China na Dunia yote. Kwenye masomo yanayofuata utasoma kwa undani juu ya utawala huu unaokuja kutawala Dunia, na viongozi 10 wa Dunia ambao watakuwa washirika wakubwa katika matukio ya siku za mwisho. Kwa sasa, angalia jinsi Babeli inavyokuwa-Ujerumani ikiiongoza Ulaya pamoja na muunganiko wa Taasisi za kidini jinsi wanavyo jibu matishio ya Urusi.
Somo lijalo utajifunza vitu ambavyo vitafungua na kukuonesha nusu ya unabii wa kibiblia.
Usisahau kusoma kitabu chote cha Danieli 4 ili uweze kuona kuwa ni kweli inasema yale uliyosoma.